Na Ahmed Abdulla
Wadau wa habari visiwani Zanzibar wamesema kuna haja ya
mabadiliko ya sheria ya habari visiwani hapa ikiwemo sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 kama
ilivyorekebishwa na sheria namba 8 ya mwaka 1997
Waliyasema hayo katika mkutano wa siku moja ulioandaliwa
na TAMWA-ZNZ kwa kushirikia na Internews Tanzania huku lengo kuu likiwa ni
kutazama baadhi ya changamoto za sheria hio.
Awali akiwasilisha mada mtalaamu wa maswala ya habari
visiwani hapa Hawra Mohamed Shamte alisema kupitia sheria hio tume ya
utangazaji Zanzibar ina uwezo mkubwa wa
kudhibiti maudhui/habari zinazotolewa na
vyombo vya habari vya kielektroniki. Hivyo, nguvu hizo zinaweza kuathiri uhuru
wa 18,vyombo vya habari katika utafutaji na usambazaji wa habari.
Akitolea mfano alisema kifungu 7(1) (b): Kudhibiti na
kusimamia shughuli za utangazaji ,tume imepewa uwezo mkubwa wa kudhibiti
mwenendo wa mtangazaji iwapo itaona kwa maoni yake mwenendo wake hauiridhishi
Tume.
Alisema neno
‘kudhibiti’ lifutwe. Sehemu inapaswa kusomeka ‘kusimamia shughuli za utangazaji.’ Sio
kudhibiti
Sambamba na hayo mtalamu huyo pia alisema neno ‘usalama’
lifutwe.’ Sehemu hiyo isomeke: “kulinda sera, utamaduni, mila na desturi za
Zanzibar”
Wakichangia mafunzo hayo baadhi ya washiriki walisema
kwa dunia ya sasa taasisi au mamlaka kupewa nafasi kubwa ya kudhibiti ni
kuminya uhuru wa watu kupata habari.
Miongoni mwa wadau hao ni Shadida Ali Omar alisema
yawezekana kwa miaka ya nyuma watu walitunga sheria hio lakini hawakutazama
mbali zaidi kwa kipindi hicho.
Alieleza kuwa kwa wakati ulipo sasa si sahihi kuwa na
sheria ngumu kiasi hicho ambazo zinakandamiza uhuru wa habari.
Alisema sheria inapaswa kuweka wazi na kutoa kipao mbele
zaiid haki ya mtu kupata na kutoa taarifa kuliko upande mmoja kujimilikisha
kama kwamba wengine hawana haki.
0 Comments