Ticker

6/recent/ticker-posts

Wadau Wataka Adhabu Ya Kifo Kwa Wabakaji

Tabia Makame-Mwandishi wa habari Zanziaba

Na Ahmed Abdulla Othman

 

Wadau wa kupambana na masuala ya udhalilishaji visiwani Zanzibar wamesema wakati umefika kwa Serikali kuweka sheria kali zaidi ikiwemo ya kuwahukumu kifo wale wote watakaobainika kuhusika moja kwa moja na kesi za ubakaji na ulawiti.

Waliyasema hayo katika mkutano maalumu wa wadau wa kupambana na udhalilishaji uliofanyika katika ofisi za TAMWA-ZNZ Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Mmoja miongoni mwa wadau hao ambae ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wajane Zanzibar Tabia Makame alisema kwa kuwa harakati mbali mbali zinaendelea kufanyika kupambana na matukio hayo anadhani njia pekee inayoweza kuzuia unyama huo ni kutolewa kwa hukumu ya kifo kwa wale wote watakaobanika.

Alisema kwa miaka mingi Zaznzibar imekua ikipambana na udhalilishaji lakini hadi sasa matukio hayo yanaendelea kutokea kila leo.

Alisema kwa kuwa matukio hayo yanaendelea kutokea licha ya wanaobainika kupewa adhabu anadhani kuna haja ya kubadilishwa kwa adhabu na sasa iwekwe adhabuu ya kuhumiwa kunyongwa akinamini ndio njia sahihi iliobakia kumaliza matendo hayo.

Awali baadhi ya wazazi walioshiriki kwenye kongamano hilo walisema kuna haja mabadiliko ya sheria hio ili watendaji wa hayo kutiwa hatiani na kupewa adhabu kali zaidi.

Kwa masharti ya kutotajwa jina mmoja miongoni mwa wazazi hao alisema ni vyema kuwekwa sharia kali zaidi na ndio njia pekee ambayo itapunguza au kumaliza kabisa matendo ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.


Post a Comment

0 Comments