Chama cha waandishiwa
habari wanawake Tanzania TAMWA kwa upande wa Zanzibar kupitia kwa mkurugenzi
wake Dkt. Mzuri Issa kimemesema kuna Umuhimu Mkubwa kwa Waandishi wa Habari
kupewa Elimu juu ya kutambua Huduma Bora wanazostahiki kuzipata Wanajamii
katika Kutekeleza Majuiumu yako ya Kila Siku.
Akifungua Mafunzo ya
Siku Nne kwa Waandishi wa Habari ya ushirikishwaji wa mwanamke katika uongozi
yenye lengo la Kutambua Haki wanazostahiki Kupatiwa Wanajamii katika Kutekeleza
Majukumu yao katika Shughuli za Maendeleo ya Jamii huko katika ukumbi wa chama
hicho Tunguu amesema jamii inapaswa kufahamu Mwenendo na Taratibu za Kijamii zinazowazunguka
Ikiwemo Suala la Kodi, Suala la Uchumi na Kutambua Sheria mbalimbali.
Hivyo amewataka
Waandishi wa Habari kufikisha Taaluma hiyo kwa Jamii ili Kusaidia Maendeleo ya jamii
na taifa kwa ujumla.
Mafunzo hayo ya Siku
nne yameandaliwa TAMWA-Zanzibar, ZAFELA,
PEGAO, kwa Udhamini wa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
0 Comments