Meneja mkuu utekelezaji wa mradi huo Amina Ussi Khamisi |
Ni mwaka mmoja sasa wa utekelezaji mradi wa viungo
visiwani Zanzibar ambapo imelezwa kuwa uwepo wa mradi huo umeleta tija kubwa na
kubadilisha maisha ya wanufaika kwa hatua ya awali.
Hayo yameelezwa na baadhi ya washiriki wa mkutano wa
siku mbili wenye lengo la kutazama fursa na changamoto za mradi huo kwa kipindi
cha mwaka mmoja wa utelezaji mradi huo.
Awali akichangia mada katika mkutano huo Bwana
shamba kutoka Wilaya ya kaskazini B Unguja Juma Kona Mosi, alisema kupitia
mradi wa viungo umewawezesha hata wao watalamu wa kilimo kufahamu kuwa kila
sehemu inawezekana kufanya kilimo cha mboga mboga na sio kama walivyokuwa
wakidhani hapo awali kuwa kilimo hicho kinahitaji maeneo maalumu tu.
Alitolea mfano shehia ya Donge kiongwe kidogo mkoa
wa kaskazini Unguja, alisema kuwa miaka mingi wao kama watalamu wa kilimo
waliamini kuwa eneo hilo halifai kuanzisha kilimo cha mboga mboga kutokana na
ardhi yake kuwa ya mchanga lakini kumbe zipo mbinu mbali mbali ambazo
zinawezesha kilimo hicho kufanya vizuri katika eneo hilo.
Alieleza kuwa kupitia elimu waliopatiwa na kisha
kuwawezesha wakulima hivi sasa ndani ya shehia ya donge kiongwe kidogo
akinamama wengi wanajihusisha na kilimo cha mboga mboga na tayari wanavuna kila
baada ya muda.
Sambamba na hilo alisema wao kama mabwana shamba
walikua na sehemu nyengine za kazi hawakuwahi kufika kutokana na
chanagmoto mbali mbali na waliami n kusingekua na haja ya kufika kutokana
na walio wengi kukosa muamko pamoja na kukata tamaa lakini hivi sasa wengi wa
watu hao wamekua wakulima na wenye kupata faida kubwa.
Nae Khadija Msonda kutoka shehia ya Mbaleni alisema
awali kabla ya ujio wa mradi wa viungo walitumia nguvu nyingi kwenye kilimo
kiasi cha kwamba kama wanawake wapo walioshindwa kutekeleza majukumu mengine ya
msingi kwenye familia zao na wakati mwengine kusababisha hata ugomvi ndani ya
ndoa.
Alisema kufuatia ujio wa mradi huo umeleta faraja
kubwa kwao kwani hivi sasa hawatumii muda mwingi kwenye kilimo lakini wanapata
faida kubwa na kuwashirikisha wengine zaidi samba nan a kuepusha migogoro
isiokua ya lazima ndani ya ndoa.
Aidha alisema inawezekana kukosekana kwa mbinu
mbadala hapo awali kuliwafanya akinamama wengi kushindwa kujikita kwenye
kilimo, waliamini kuwa wasingeweza kunufaika badala yake walijikita na shughuli
nyengine zikiwemo kilimo cha mwani lakini, hivi sasa watu wengi wamehamasisha
na wamejikita kweye mradi huo.
Mkulima msaidizi Khadija Msonda kutoka shehia mbaleni kitope akieleza jinsi mradi wa viungo ulivyoweza kummbadilisha na kuwasaidia wengine katika jamii yake. |
Nae Amina Kheri alisema ndani ya mwaka mmoja wa
utekelezaji mradi huo umewaamsha akinama wengi kufahamu umuhimu wa kulima na
kula mboga mboga kinyume na ilivokua mwanzoni.
Alisema licha ya mradi huo kujikita na kilimo
lakini pia utapunguza kwa kiasi kikubwa wimbi la akinamama wanaohitaji damu
wakati wa kujifungua baada ya kujiwekea utaratibu wa kula mboga mboga
wanazolima kwa muda na siku wanayotaka wenyewe.
Awali akifungua mkutano huo meneja mkuu utekelezaji
wa mradi huo Amina Ussi Khamis aliwataka washiriki wa mkutano huo kutumia fursa
hio kueleza yale walioyaona na kupendekeza mambo gani mapya yafanyike kwa mwaka
wa pili ili kuongeza kasi ya uzalishaji na mafanikio zaidi kwa wakulima na
Serikali kwa ujumla.
Mkutano huu wa siku mbili unaofanyika katika ofisiz
za utekekelezaji mradi huo Mwanakwerekwe mjini hapa ,umewashirikisha mabawana
shamba pamoja na wakulima wawezeshaji wapata 72 kutoka maeneo mbali mbali ya
Unguja kupitia mradi wa Viungo ambao unafadhiliwa na umoja wa Ulaya na
kutekelezwa na PDF,TAMWA,ZNZ pamoja na CFP huku ukilenga kuwafikisha wanufaika
57,000 kutoka Unguja na Pemba.
0 Comments