Wakati Dunia na Tanzania kwa ujumla ikiwa bado katika
maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa amesema
maadhimisho hayo yanapaswa pia kutazamwa hali ya usawa wa kijinsia kwa
wanahabari visiwani hapa kwa kuwa bado wapo baadhi ya wanahabari wanawake
wamekua wakikabiliwa na majaribu ya rushwa na ngono wanapoomba ajira.
Aliyasema hato katika mkutano maalumu uliolenga kutazama
hali ya uhuru wa habari na umuhimu wa uwepo wa sheria bora ya habari visiwani
hapa katika mkutano ulioandaliwa na shirika la Intenrnews Tanzania kupitia
mtandao (Zoom)
Alisema hadi sasa vyombo vingi vya habari pande zote
mbili za Tanzania hawana sera ya jinsia ambayo wanatumia badala yake hufanya
kazi kimazoea na kupelekea wanawake wengi kubaki kuwa nyuma na kukutana na
chanagamoto mbali mabali zikiwemo za kudaiwa rushwa ya ngono.
Alisema uwepo wa sera ya jinsia kwenye vyombo vya habari
ungeweza kuweka bayana namna gani wanahabri na vyombo vyao wanatakiwa kufanya
kazi na wanawake kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyo alizungumzia
kuhusu kukosekana kwa uwajibikaji katika
vyombo vingi vya habari zaidi katika suala la mishahara kwa wafanyakazi wao.
Akifafanua zaidi alisema rushwa za ngono hujitokeza
zaidi wakati wa ajira kwenye vyombo vya habari na ndipo wasichana wengi
hujikuta wanaingia kwenye mtego na wapo wanaoamua kufanya jambo hilo wakiamini
ndio njia pekee ya kupata ajira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha huduma za sharia
Zanzibar Harous Mpatani wakati wakati akiwasilisha mada katika mkutano huo
aliema haki ya kupata habari ni ya kikatiba na kila anapaswa kupata haki hio
bila ya kuminywa.
Alieleza Zanzibar kama sehemu ya dunia imeridhia
mikataba ya kimataifa ikiwemo wananchi wake kupata na kutoa habari hawana budi
kuheshimu mikataba hio.
Akichangia katika kongamano hilo mwanahabari mwandamizi
kutoka Zanzibar Hassan Issa alisema anasikitishwa sana kukosekana kwa umoja
katika tasnia hio kiasi ambacho wapo watu Fulani wanaojiona wao bora na kuwaona
wengine ni watu wasiokua na maana wakati wote ni wanataaluma sawa.
Alisema tabia za kusemana vibaya na wakati mwengine hata
mtu au watu kuwaandalia wenzao mabaya si jambo zuri na linapaswa kuachwa kwa
maslahi ya taaluma hio na watu kurudi kuwa kitu kimoja.
Wakati akifunga mdahalo huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Khamis Abdalla Said amesema ili
mabadiliko katika sekta ya habari yaweze kutokea hakuna budi kuwepo kwa umoja
kwa wanadao wote na Serikali.
Alisema suala la umoja na mshikamano ni jambo zuri
katika kila sehemu na kutokubali kugawiwa wao wenyewe watajikuta wakiwa katika
kufanikisha mipango yao pasipo na kutoa malalamiko.
Sambamba na hayo
alisema wizara imetakiwa kuzifanyia mapitio baadhi ya sheria na kuwataka
waandishi wa habari habari kupeleka mapendekezo yao kwa sheria ambazo wanaziona
ni kandamizi kwao.
“Kwa ukweli kabisa ni kwamba Serikali imesikia kilio
chenu na ndio maana ikatoa ruhsa mulete mapendekezo ya sera kwa lengo la kupata
sharia bora ya habari ambayo italeta manufaa kwa pande zote mbili” alisema.
Hata hivyo alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto za
kisheria lakini haiwezekani kuachiwa
watu kufanya wanavyotaka kwa kuwa kila uhuru una mipaka yake.
Alifahamisha kwamba ni wakati sasa wakaitumia hiyo fursa
ya wadau hao wa habari kuziainisha sheria ambazo wanaona zinahitaji kufanyiwa
marekebisho badala ya kukaa tu na kulalalamika.
0 Comments