Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja Mh. Rashid Hadid Rashid akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha chwaka katika kikao cha kusikiliza changamoto za wananchi wa kijiji hicho
Wananchi wa kijiji cha Chwaka wilaya ya Kati wameiomba serekali ya mkoa kusini kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili ikiwemo ukosefu wa huduma ya maji safi na salama pamoja na baadhi ya vipimo vya afya kwa mama wajawazito.
Wakizungumza huko Chwaka katika kikao cha pamoja kati ya viongozi wa mkoa na wilaya ikiwa ni muendelezo wa ziara waliyojipangia kwa kuzipitia shehia zilizomo ndani ya mkoa huo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Wananchi hao wamesema licha ya kuwepo kituo cha afya katika maeneo hayo kinachoendelea kutoa huduma kila siku lakini pia hulazimika kufuata huduma za mama wajawazito katika vituo vyengine hali inayowapa usumbufu mkubwa kulingana na hali zao.
Aidha wananchi hao wamesema
wanakabiliwa na tatzo la uhaba wa madarasa na huduma ya miaji safi na
salama ambayo hulazimika hata kununua au kutoka nyakati za usiku
hali inayopelekea kurudisha nyuma juhudi za maendeleo kijijini hapo.
wanannchi wa kijiji cha Chwaka wakisikiliza ufafanuzi wa changamoto zao kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja Mh. Rashid Hadid Rashid katika kikao cha kusikiliza changamoto za wanakijiji wa kijiji hicho
Mkuu wa mkoa wa Kusini Ungija Mh. Rashid Hadid Rashid ameahidi kwa kusema kuwa serekali itahakikisha inayatafutia ufumbuzi matatizo hayo na kuwasisitiza wanachi hao kuisaidia serekali kupambana na vitendo vya udhalilishaji pamoja na masuala ya kujihusisha na uvuvi haramu ambavyo vinaonekana kuendelea kushamiri siku hadi siku.
Hata hivyo amewafahamisha wananchi
wa kijiji hicho kwamba umefika wakati sasa kulipa umuhimu wa kipekee suala la
kutunza mazingira na kulinda rasilimali za bahari kwani kufanya
hivyo kutaleta maslahi kwa pande zote na pia kuvinufaisha vizazi vya
baadae.
0 Comments