Mashindano ya mimi na wewe mapinduzi
nage cup yamefikia tamati kwa mchezo wa fainali uliowakutanisha mahasimu wawili
wa mji wa karakara kwa maana ya timu ya Karakana United wakipambana na Karakana Rengers.
Katika mchezo huo wa vuta
nikuvute ulishuhudiwa kwa timu ya Karakana
United kuongoza kwa mabao 20 huku timu ya Karakana Rengers ikipata mabao 9 hivyo kuifanya timu ya karakana
united kuwa bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu wa 2021.
Awali Waziri Wa Habari Vijana
Utamaduni Na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita alipata nafasi ya kuzungumza na
wanamichezo pamoja na wadau wa mchezo huo ambapo aliwataka kuwa na mashirikiano
na kutokuwa na uhasama wa kimichezo kwani kufanya hivyo kutapelekea maendeleo
ya mchezo huo pamoja na chama cha mchezo huo kwa ujumla.
“Michezo ituunganishe na
kutuongezea mshikamano na upendo hususan michezo hii tunayoicheza kwa ajili ya
kudumisha kumbukumbu ya mapinduzi” alisema waziri huyo
Aidha aliahidi kuwa atahakikisha chama cha mchezo
wa nage za Zanzibar kinapatiwa usajili kwa gharama inayoendana na udogo wake
ili kuona chama hicho kinakuwepo kwa mujibu wa taratibu na sharia zilizowekwa.
“Naahidi usajili utapatikana
kwa wakati kabisa na nitamuelekeza mwanasheria wangu atalichukuwa na kulifanyia
kazi” alisema Mhe Tabia
Sambamba na hayo ameahidi
kusaidia chakula cha siku zote watakazokaa katika kambi huko Kinondoni Jijini Dar
es salam ikiwa ni hatua za kubadilishana mawazo kwa wanamichezo wa mchezo huo
wa visiwani Zanzibar na wenzao wa Dar er salam.
“Mhe. Mbunge ameahidi
kugharamia gharama za usafiri kwa wale watakaobahatika kwenda Dar es salam na
mimi waziri wenu nitadhamini chakula cha siku zote mtakazokuwa kule Kinondoni”
aliongezea waziri huyo
Katika hatua hiyo alimuagiza
Raisi wa chama cha mchezo wa nage Zanzibar kuhakikisha usalama wa wanamichezo
hao wakiwa katika safari na kambi yao huko Jijini Dar es salam ambapo aliahidi
kufuatilia kwa karibu safari hio ili kuona wanamichezo hao wanakuwa salama
katika safari yao hiyo.
“Raisi wa chama cha nage una
jukumu kubwa kuhakikisha usalama wa mabinti wetu unakuwa wa kutosha
nitafuatilia kwa karibu mwenendo wa safari hiyo” alisisitiza mhe. Tabia
Kwa upande wake Raisi wa
chama cha mchezo wa nage Zanzibar Haji Kaka alisema watahsakikisha chama
kinasimamia mchezo huo ili kuona unakuwa ni sehemu ya ajira kwa wanamichezo wa
mchezo huo.
“Tutahakikisha tunausimamia
mchezo huu ili iwe ni sehemu ya ajira kwa wanamichezo wetu” alisema Haji Kaka
Ashura kudura mohammed ni
nahodha wa timu ya Karakana United alisema siri kuu ya ushindi wao ni kujituma katika
kufanya mazoezi pamoja na kutekeleza maagizo ya kocha wao ambapo amewataka
wanajamii kuachana na dhana ya kuwa mcheozo wa nage ni mchezo wa kihuni.
“Tumefanya mazoezi kwa bidii
pia tumezifuata mbinu zote za mwalimu na ndio mana tumepata matokeo haya”
alisema Nahodha huyo
Kwa upande wa mchezaji wa
timu ya Karakana Rengers Salma
Othman Omar alisema kupoteza kwa mchezo wao huo wa fainali kumesababishwa na
kuzuiliwa kwa baadhi ya wachezaji wao tegemezi hivyo imewapelekea kutoka katika
ubora wao na kupoteza mchezo huo kwa mabao mengi.
“wachezaji temecheza nao
katika michezo iliyopita ila katika fainali wanazuiliwa kwa hili hatujatendewa
haki” alisema Salma Othman
Mashindano hayo hufanyika
kila mwaka ikiwa ni katika harakati za kudumisha historia ya Mapinduzi matukufu
ya 1964.
0 Comments