Umoja wa Vyama Vya Siasa visivyo rasmin vimempongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kumteuwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Akizungumza na Waandishi wa habari huko katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar Katibu wa Umoja wa vyama vya siasa visivyo rasmin Ameir Hassan Ameir amesema hatua aloichukua Rais ni yakupongezwa na ni yakisheria.
Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa kutimiza kauli zake za kuunda Serikali ya Kitaifa wakati wa kampeni zake .
Nae Makamo Mwenyekiti Peter Aghaton Magwira ameeleza kuwa watatekeleza kwa vitendo katika kumsaidia Rais wa Zanzibar yale yote yanayofaa ili kuleta maendeleo katika Nchi.
Hata hivyo amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa kufata sheria na watamuunga mkono ili kuendeleza kuilinda amani iliyopo katika Nchi hiyo.
“Tutaendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria na kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ili kuleta maendeleo na kulinda amani ya Nchi”alisema katibu wa Umoja huo.
Vile vile waliwaomba Viongozi wote na Wananchi kwa Ujumla kushirikiana kwa pamoja ili kuzidi kuleta maendeleo ya Zanzibar .
0 Comments