Makamu wa kwanza wa
rais wa zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar haitomvumilia mtu yeyote ambaye ataleta uchochezi wa kuwagawa
wananchi na kuanzisha hasama miongoni mwao.
Amewataka wananchi Kudumisha
Amani Na Umoja uliopo na kukataa vitendo vya wale wanaopinga umoja uliopo
Nchini kwani kufanya hivyo kutapelekea kuipatia Zanzibar Maendeleo kwa haraka.
Maalim Seif aliyasema
hayo alipojumuika na Waumini Wa Dini Ya Kiislam katika Ibada Ya Sala ya Ijumaa
Katika Msikiti Wa Ar Rahma Uliyopo Bububu Kijichi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Maalim seif ambaye pia
ni mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo alisema wako watu ambao hawaridhishwi
na mshikamano unaofanywa na wanachi jambo ambalo linaweza kuzorotesha ukuwaji
wa maendeleo katika taifa.
Alisema kuwa kuwepo
kwa umoja na mashirikiano ya wananchi ni jambo la muhimu katika nchi na
kuwataka watu waachane na ubaguzi kwa kuangalia itikadi za kisiasa katika
masuala ya kusimamia maendeleo yao.
“Kama tukiwa wamoja ni
rahisi nchi yetu kupiga hatua za kimaendeleo katika Nyanja zote na kuwa mfano
wa nchi nyingi za Afrika” alieleza Maalim Seif.
Sambamba na hilo
Makamu wa Kwanza wa Rais aliwataka wananchi kuacha ubaguzi wa rangi au wa
kisiasa kwani mbora kwa mwenyezi ni Yule mchaji zaidi.
Maalim Seif alisema
dhamira ya yeye na Rais wa Zanzibar Dr. Husein Ali Hassan Mwinyi ni kufanya kazi
kwa pamoja ni kuondoa changamoto ambazo hupelekea wananchi kutofautiana na
kuleta chuki miongoni mwao.
“Tumeunda serikali hii
ya shirikishi ili hasama na chuki zoote zinazosababishwa na uchaguzi
zisijirudie tena kwani hazi tija wananchi wetu” alieleza maalim Seif.
Alisema kuwa
wazanzibar watakuwa wamoja vitendo vyoote viovu vitakuwa historia pamoja na
vurugu zinazotokea katika kipindi cha uchaguzi.
Alisema kuwepo kwa
Serikali yenye muundo wa umoja wa kitaifa ni njia moja ya kubaini sababu ya
kupata dawa kulinda Zanzibar isirejee tena katika migogoro isio yan lazima.
Maalim Seif alisema
wazanzibar wamebahatika pia kupata dini ya Kislamu ambayo katika maeneo mengi
inasisitiza umoja miongoni mwa jamii ya Waslamu kwa wazanzibar asiliimia
kubwa ni waumini wa dini hiyo.
“Tumuombe mwenyezi
Mungu atulinde na maaduwi ambao hawapendi umoja wetu” alieleza Maalim Seif.
0 Comments