Inter Milan itaanza
mazungumzo na aliyekuwa mshammbuliaji wa Everton na Manchester United Romelu
Lukaku juu ya mkataba mpya huku timu kadhaa zikimnyatia mshambuliaji huo wa
Ubelgiji ikiwemo Juventus. (90 Min)
Aliyekuwa mshambuliaji
wa Liverpool na Manchester City Mario Balotelli yuko tayari kusaini mkataba na
klabu ya Serie B ya AC Monza katika makubaliano ya hadi mwisho wa msimu.
Mchezaji huyo, 30, amekuwa bila klabu tangu alipoondoka Brescia timu hiyo
iliposhushwa daraja msimu uliopita. (Sky Sports)
Manchester United iko
tayari kumzawadi kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 26, mkataba mpya
ambao mshahara wake utaongezwa mara mbili na kufikia kima cha pauni 200,000 kwa
wiki na kumaliza jitihada za Barcelona na Real Madrid waliokuwa pia
wanamkodolea macho. (Sunday Mirror)
Timu kadhaa za Ligi ya
Premier na Scotland zinamnyemelea Jesse Lingard
Kiungo wa kati wa
England Jesse Lingard, 27, yuko tayari kuiomba Manchester United imruhusu
kuondoka Januari, huku klabu kadhaa za Ligi ya Premier na zile za Scotland za
Rangers na Celtic zikisemekana kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (Team Talk)
Hata hivyo, Manchester
United iko tayari kuongeza mkataba wa Lingard kwa mwaka mmoja zaidi - licha ya
kuendelea kukosekana katika timu ya kwanza. (Star on Sunday)
Mlinzi John Stones
akipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mchuano
Kocha wa Arsenal Mikel
Arteta ameitaka iliyokuwa klabu yake Manchester City kuendelea kumfahamisha
kuhusu upatikanaji wa mlinzi wa England John Stones, 26. (90 Min)
Mkurugenzi wa Paris
St-Germain Leonardo anasema klabu hio inapiga hatua wakati inapoendelea
kutafuta mbinu za kumshikilia mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21.
(Goal)
Jose Mourinho anasema
Tottenham "haikupoteza muda wetu" kujaribu kumsajili kiungo wa kati
wa Brazil Willian, 32, kwasababu hawakuweza kufikia ofa ya Arsenal. (London
Evening Standard)
Leicester City
imehusishwa na winga wa Sporting Lisbon raia wa Ecuador Gonzalo Plata, 20. (Vitotvo,
via Leicester Mercury)
Aliyekuwa mlinzi wa
Liverpool Conor Coady, 27, beki wa kati wa Wolves na England, alijua kuwa
aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Molineux na mshambuliaji wa Ureno Diogo Jota,
24, ataonesha matokeo chanya haraka mno Anfield. (Liverpool Echo)
Na mechi ya Newcastle
dhidi ya West Brom Jumamposi ijayo ipo "mikoni mwa wahudumu wa afya",
kulingana na kocha wa Baggies Slaven Bilic. (Newcastle Chronicle)
Na haimae Rais wa
Besiktas Ahmet Nur Cebi amekubali kufuatilia kwa karibu kumsajili tena
mshambuliaji wa Everton raia wa Uturuki Cenk Tosun, 29, lakini amedokeza kuwa
upande wake unaweza tu kufikia makubaliano ya mkopo. (Liverpool Echo)
Kocha wa Real Madrid
Zinedine Zidane amewasiliana na kiungo wa kati wa RB Salzburg raia wa Hungary
Dominik Szoboszlai, 20, akiwa na matumaini ya kumshawishi akubali usajili wa
klabu hiyo ya Uhispani. (Bild, via AS)
Timu ya Serie A ya
Bologna inamnyatia mshambuliaji wa Wolves Patrick Cutrone, 22, raia wa Italia
ambaye sasa hivi yuko kwa mkopo Fiorentina. (Il Resto del Carlino, via Sport
Witness)
0 Comments