Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesisitiza wafanyakazi wa wizara hiyo kufanya Kazi kwa Ubunifu na Usahihi ili kuona kwamba wananchi wananufaika na Rasilimali za taifa lao.
Dkt. Kalemani
ameyasema hayo Desemba 12, 2020 katika kikao kazi cha kwanza kilichojumuisha
Wakuu wa Bodi, Menejimenti, Idara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya wizara
hiyo kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa kiserikali Mtumba
Dodoma kilichokuwa na lengo la kufahamiana na kutoa maagizo na maelekezo
mbalimbali ya msingi ambayo yanapaswa kutekelezwa katika Serikali ya awamu hii.
“Nimewaita kwa mambo
mawili tu, jambo la kwanza ni kufahamiana ndilo jambo lililonifanya niwaite
wajumbe wa bodi zote za wakurugezi na menejimenti pamoja na uongozi wa wizara
na kufahamishana mambo ya msingi ya kufanyia kazi na jambo la pili ni
kuwaarifu kuwa tumeanza kufanya kazi na kikao hiki sio kikao tu bali ni kikao
cha kwanza cha kazi” Alisema Kalemani
Dkt. Kalemani alielezea utekelezaji wa kauli mbiu itakayotumika kwa kipindi cha miaka mitano
ambayo ni Kasi, Ubunifu na Usahihi na amezidi kuwataka watumishi wote wa Wizara
hiyo kufanya kazi kwa kasi kubwa huku wakizingatia ubunifu na kwa usahihi wa
kazi huku akiwaasa watumishi hao kutimiza wajibu wao na akaendelea kutoa rai
ya kupambana na mtu ambaye hatatimiza wajibu wake katika kazi.
“Nitangulie kusema
tunakwenda na kauli mbiu ifatayo, ndio kaulimbiu yetu kwa miaka hii mitano ya
kipindi cha pili cha awamu ya tano. Kauli mbiu yetu ni Kasi, Ubunifu na
Usahihi, kila mmoja atakachoelezwa hapa akifanye kwa kasi kubwa, Ubunifu na
Usahihi” Alieleza Waziri huyo
Dkt. Kalemani
aliongezea kwa kuliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wahakikishe
wanatekeleza majukumu yao yote kwa ufasaha huku akiwaagiza wakurugezi wote wa
Shirika hilo nchi nzima kuendelea kushugulikia na kutatua kero mbalimbali kama
kukatika kwa umeme mara kwa mara na kero nyingine pamoja na kuhakikisha miradi yote
inayosimamiwa na Shirika hilo inatekelezwa kwa wakati.
Aidha, Dkt. Kalemani
aliendelea kutoa maagizo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kukata umeme
kwa wadaiwa wote nchi nzima bila kujali Taasisi binafsi wala Taasisi za umma
huku akiwataka wakurungezi wote kuhakikisha wanakusanya mapato kutoka kwa
wateja wao.
“Lazima TANESCO
tukusanye mapato kutoka kwa wateja wetu maana jana nilipoingia ofisi nimepokea
taarifa mpaka sasa tunadai zaidi ya Bilioni 182 kwa Taasisi za umma na wateja
wa kawaida Bilioni 3.6, Mwenyekiti wa bodi nakuagiza kwa tunaemdai kata umeme,
acha nilaumiwe mimi kwanza, kwahiyo kuanzia leo kama kuna mteja au Taasisi iwe
ya Umma au ya binafsi tunayoidai naelekeza kwa bodi ya TANESCO katieni umeme
kuanzia leo”
Nae Naibu Waziri wa
Nishati, Mhe. Stephen Byabato aliendelea kuwasisitiza watumishi wote wa Wizara
hiyo kutimiza wajibu wao huku akiwasihi kutekeleza kikamilifu maelekezo yote
yaliyotolewa na Waziri na yatakayoendelea kutolewa na viongozi wa Wizara hiyo
na Serikali nzima kwa ujumla.
0 Comments