OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, siku
ya jana amefunga ndoa na mkewe Naheeda, katika msikiti wa Masjid Maamur.
Katika Ndoa yake huyo ilihudhuriwa
na watu mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete,
Sheikhe Mkuu wa mkoa wa Dar, Alhad Mussa Salum na watu wengine wengi maarufu.
Katika nasaha zake Raisi mstaafu
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Kikwete alisema kuwa Haji alimfuata
nyumbani na kumshirikisha jambo hilo kwa ajili ya ndoa na akamuahidi kuja.
Aidha Dkt. Kikwete alisema katika
ndo hakuna ufundi isipokuwa jambo pekee na la muhimu ni kuvumiliana kutokana na
kasoro za kila mwanandoa.
“Hakuna ufundi kwenye ndoa kikubwa
ni kustahimiliana na kuvumiliana kwa kuwa hakuna ufundi katika ndoa” alisema
Dkt. Kikwete
Vilevile Dkt. Kikwete aliendelea
na nasaha zake kwa Wanandoa hao aliwataka wawe makini katika ndoa kwa kuwa na
msimamo wa kuaminiana sambamba na kuweza kulea vyema vizazi vyao kwa maadili
mema pale watakapojaaliwa kupata vizazi hivyo.
"Mnapaswa kuwa makini na
kuskilizana katika ndoa, pia nakushauri ujue kwamba uwe na uvumilivu na kuona namna
gani mnaweza kuleta watoto kwa kuulizana na kujua mambo yatakuaje”
Alisema katika suala hilo la
kupata kizazi ni kazi ya Muumba mwenyewe hivyo wawe na subira hadi pale
watakapojaliwa kupata kizazi.
"Baraka za Mungu kwa watoto
ni zake ka kadri atakavyoamua, yale makundi yaache kwa kuwa kila mmoja anajua
anachokipenda”
"Nilikuwa ninazungumza na
mzee hapo nyuma akaniambia kwamba anahitaji wajukuu hivyo ni jambo la kheri na
linahitaji subira kikubwa ninawapongeza katika hilo na ninaamini kwamba itakuwa
kheri," amesema.
0 Comments