Ligi kuu ya Zanzibar
ZPL itaendelea leo Disemba 11 kwa michezo mitatu katika viwanja tofauti
kisiwani Unguja.
Mchezo wa kwanza
utachezwa katika kiwanja cha Amani majira ya saa 10:00 za alaasiri kwa timu ya
black sailor watakapoikaribisha timu ya police
Katika mchezo uliyopita ikiwa ni wa mzunguko watatu timu ya Black Sailor ambayo ipo nafasi ya
5 ikiwa na alama zake 4 ikiwa imeshacheza jumla michezo mitatu ilipoteza kwa
kufungwa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Malindi huku timu ya Police ambayo
inashikilia mkia ikiwa nafasi ya 12 ikiwa na alama yake 1 ikiwa imecheza
michezo yake mitatu ilikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya timu ya
Zimamoto.
Mchezo mwengine ambao
utapigwa leo hii ni mchezo kati ya timu Chuoni dhidi ya timu ya Mlandege ambao
utapigwa majira ya saa 10:00 za alaasiri katika kiwanja cha Mao A.
Mchezo uliopita timu ya
Chuoni ambayo ipo nafasi ya 10 ikiwa na alama yake 1 ikiwa imeshacheza michezo
yake miwili ilitoa sare ya 0-0 dhidi ya timu ya timu ya Black Sailor ambapo
timu Mlandege ambayo ipo nafasi ya 7 na alama zake 3 ikiwa imeshacheza michezo
miwili ilipoteza mbele ya timu ya Kipanga kwa kufungwa bao 1-0.
Pia katika Dimba la Mao
B kutakuwa na mchezo kati ya Malindi dhidi ya KVZ majira ya saa 10:00 za
alaasiri, ambapo katika mchezo uliopita timu ya Malindi ambayo ndio vinara wa
ligi kuu ikiwa na alama zake 9 kibindoni ikiwa imeshacheza michezo mitatu
ilipata ushindi mnene wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Black Sailor huku timu ya
KVZ ikiwa ipo nafasi ya 8 ikiwa na alama zake 3 na imeshacheza michezo miwili
iliishinda kwa kuifunga timu ya Hard Rock mabao 3-2.
0 Comments