Jamii nchini imeshauriwa
kuwa na muamko katika mambo ya kujitolea ili kuhakikisha mabadiliko ya kiuchumi
na kujamii yanaimarika siku hadi siku.
Hayo yalielezwa na
mratibu mkaazi wa shirika la kujitolea la
umoja wa mataifa la UNV anayefanya kazi zake nchini Tanzania, bwana Christian Mwamanga wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habar huko katika hoteli ya Verde iliyopo Mtoni
wilaya ya mjini unguja.
Alisema suala la
kujitolea kwa wanajamii linachangia kwa kiasi kikubwa ukuwaji wa uchumi katika
mataifa mbalimbali licha ya baadhi ya wanajamii wengi kutoitumia fursa ya
kujitolea na badala yake wakiwa wameelekeza kufanya kazi zenye kuwapatia malipo
jambo ambalo hurejesha nyuma jitihada za wanaojitolea.
“endapo jamii ikiw na
muamko wa kujitolea tutapiga hatua kubwa ya maendeleo yetu tuwe wazalendo wa
kujitolea tusitegemee sana kulipwa” Alisema Bwana Christian
Aidha alisema shirika
la kujitolea duniani la UNV limekuwa likifanya mambo mengi kuzisaidia jamii
ambapo alisema zaidi ya watu bilioni moja duniani wanafanya kazi za kujitolea huku
asilimia 70 kati yao ni wale ambao wanafanya kazi katika sekta zisizo rasmi na
asilimia 30 ndio ambao wanafanya kazi katika sekta zilizo rasmi.
“Kuna zaidi ya watu
bilioni moja wanaojitolea duniani asilimia 70 kati yao wanafanya kazi katika
sekta zisizo rasmi na asilimia 30 pekee ndio wanafanya kazi katika kekta zilizo
rasmi” Aliongezea mratibu huyo
Alisema katika kipindi
ambacho dunia imekumbwa na janga la COVID-19 watu wanaojitolea pia wamekubwa na
janga hilo duniani kote ambapo licha ya kukumbwa kwao na janga hilo pia
walichangia jitihada zao katika kupambana kikamilifu na janga hilo.
“Kwa mwaka huu dunia
imekuwa na janga la virusi vya Corona kama watu tunaojitolea hatukunusurika” Alieleza
Alipozungumzia siku ya
kujitolea duniani alisema kwa mwaka huu maadhimisho yake kitaifa yatafanyika
Zanzibar katika kijiji cha Nungwi hapo kesho ambapo aliwataka wananchi wote
kujitokeza kwa wngi katika maadhimisho ya sherehe hizo.
Alisema katika maadimisho
hayo shughuli mbalimbali za kijamii zitakuwepo zoezi la uchangiaji damu wa
hiari,mazungumzo ya kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika suala la kujitolea
pamoja na michezo mbalimbali.
“Niseme tu kilele cha
sherehe ya siku hii ya kujitolea duniani tukuwa na shughuli mbalimbali ambazo
tutazitekeleza hapa Zanzibar tuchangia damu,tutazungumza mafanikio ya kujitolea
pamoja na michezo” Alifafanua mratibu huyo
Siku ya kujitolea
duniani husherehekewa duniani kote kila ifikapo tarehe tano Dicemba ambapo kauli
mbiu ya mwaka huu ni "kwa pamoja tunaweza kuleta maendeleo endelevu Katika
kujitolea.
0 Comments