Vijana nchini
wametakiwa kuwa na utaratibu wa kujitolea katika mambo ya maendeleo ili
kuisaidia serikani kuinua uchumi wa taifa.
Wito huo ulitolewa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa, Serikali za mitaa na Idara
maalumu za SMZ mhe, Masoud Ali Mohammed katika maadhimisho ya sherehe ya siku
ya kujitolea duniani iliyofanyika huko katika hoteli ya Kendwa Rock.
Alisema vijana wana
nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya taifa hivyo endapo wa watajitolea
katika kupiga vita rushwa,ubadhirifu wa mali za umma pamoja na vitendo vya
udhalilishaji itapelekea ukuaji wa uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha alisema Siku ya
wanaojitolea duniani ni fursa adhimu kwa kila mmoja kuendeleza moyo wa
kujitolea hivyo ameyaomba mashirika ya umoja wa mataifa jumuiya zisizo za
kiserikali pamoja na serikali kuweza kuunga mkono juhudi za wale wanaojitolea
na kutambua umuhimu wa michango yao wanayoitoa kwa Taifa.
Mwanaid Mohd ni
mkurugenzi wa idara ya vijana na maendeleo amesema serikali itaendelea
kuzithamini jitihada za vijana wanaojitolea kwani wana uwezo mkubwa wa
kuchangia na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo ya nchi.
Kwa upande wao vijana wanaojitolea kutoka mashirika na tasisi
mbalimbali wamesema Lengo la kujitolea ktk tasisi na mashirika hayo ni kuweza kuonesha
watu wa makundi tofauti kuweza kupigania maendeleo ya taifa katika kuhakikisha
wanaleta mageuzi ya kiuchumi katika jamii na taifa kwa ujumla.
Akitoa neon la
shukurani mratibu mkaazi wa shirika la kujitolea
la umoja wa mataifa la UNV anayefanya kazi zake nchini Tanzania, bwana
Christian Mwamanga ameishukuru serikali pamoja na wananchi wote kwa
kushirikiana katika maadhimisho hayo huku akiwataka wananchi hao kuwa mabalozi
wazuri kwa kuwaelimisha wananchi ambao hawakufika katika sherehe hizo umuhimu wa
kujitolea katika taifa.
Siku ya wanaojitolea
duniani hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 5 disemba na ujumbe wa mwaka huu ni
kujitolea kwa pamoja unawaza.
0 Comments